Ramani ya
mpaka wa Kenya na Tanzania
|
Kenya
imeilaumu Tanzania kwa kuwaweka raia wa Ethiopia katika eneo lake la mpaka siku
ya Jumanne badala ya kuwarudisha makwao kulingana na ripoti ya gazeti la The
standard nchini Kenya.
Raia hao
wa Ethiopia walikuwa wamewachiliwa huru baada ya kuhudumia vifungo vya mashtaka
tofauti ya uhalifu nchini Tanzania.
Maafisa
wa polisi wameagizwa kutowaruhusu wageni hao kuingia nchini Kenya.''Watarudishwa
nchini Tanzania walikotoka.
Kisa
hicho hakikubaliki na hakiruhusiwi na sheria'',Afisa wa Kenya Henry Wafula
alinukuliwa akisema.
chanzo bbc swahili
No comments:
Post a Comment