Mahakama
ya Kenya imemhukumu adhabu ya kifo Bw. Thabit Jamaldin Yahya, mtuhumiwa mkuu wa
shambulizi la kigaidi lililotokea katika klabu ya Bella Vista mjini Mombasa
mwezi Mei mwaka 2012, na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Jaji
wa mahakama hiyo Martin Muya amesema, sampuli ya DNA ya Bw Yahya iliyotolewa na
Shirika la upelelezi wa Marekani FBI, inalingana na damu iliyogunduliwa
katika sehemu lilipotokea shambulizi.
Mwanasheria
wa Yahya amesema atakata rufaa. Polisi wa Kenya wamesema Bw. Yahya ni mpiganaji
wa kundi la Al-Shabaab, ambalo limefanya mashambulizi mengi nchini Kenya.
chanzo idhaa ya Kiswahili china
Wow .... keep it up
ReplyDelete