Tetemeko la kwanza lilitokea Alhamisi wiki iliyopita
|
Watu
karibu 250,000 wametakiwa wahame kutokana na wasiwasi wa kutokea kwa mitetemeko
zaidi ya ardhi nchini Japan, shirika la kutoa misaa limesema.
Naoki
Kokoawai, mshauri wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Japan, ameambia BBC kwamba
makundi zaidi ya matabibu yanatumwa maeneo ya kusaidia waathiriwa.
Mitetemeko
miwili mikubwa ilitikisa kisiwa cha kusini magharibi cha Kyushu wiki iliyopita
na kuua watu 42.
Idara ya
utabiri wa hali ya hewa imetahadharisha kwamba kuna uwezekano mkubwa wa
mitetemeko zaidi huenda kutokea siku chache zijazo.
Watu
zaidi ya 1,000 walijeruhiwa na miundo mbinu mingi kuharibiwa.
Wafanyakazi
karibu 30,000 wa uokoaji wanasaidia kutafuta manusura. Polisi wamesema watu 11
bado hawajulikani walipo, kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali la
NHK.
"Bado
kuna watu ambao hawajulikani walipo. Tunataka kufanya juhudi zaidi na kuwaokoa
watu,” Waziri Mkuu Shinzo Abe aliambia Bunge mapema Jumatatu.
Nyumba nyingi zimebomoka
Mwanamke
wa umri wa miaka 61 alipatikana akiwa amefariki karibu na nyumba yake
iliyoporomoka eneo la Kumamoto mnamo Jumapili, gazeti la Japan Times
liliripoti.
Tetemeko
la ardhi la nguvu ya 7.3 lilitokea karibu na jiji la Kumamoto, ambalo lilikuwa
limeathiriwa na tetemeko jingine la nguvu ya 6.4 Alhamisi usiku.
Mitetemeko
hiyo miwili ilisababisha uharibifu mkubwa.
Jeshi la
Marekani limesema liko tayari kutoa usaidizi wa ndege kusaidia juhudi za uokoaji.
chanzo bbc swahili
No comments:
Post a Comment