Majimbo matano nchini Marekani yanapiga kura kumteua mgombea atakayewania urais kupitia tiketi ya vyama vyao.
Uchaguzi
huo huenda ukawapa fursa wagombea wa vyama vya Democrat na Republican
kuimarisha uongozi wao.
Kura
zimeanza kupigwa katika jimbo la Ohio na Florida yote yakionekana kuwa muhimu
pamoja na majimbo ya Carolina Kaskazini ,illinois na Missouri.
Mgombea
wa chama cha Democratic aliye kifua mbele Hillary Clinton atatumai kwamba
atafanikiwa kum'bwaga mpinzani wake wa karibu Bernie Sanders .
Wakati
huohuo Donald Trump atalenga kuwaangusha wapinzani wake katika kinyang'anyiro
hicho.
Bilionea
huyo anapigiwa upatu kushinda uteuzi wa mgombea wa Republican lakini
anakabiliwa na upinzani katika chama cha Republican pamoja na chama cha
Democrats.
Aliandikisha
ushindi wa mapema siku ya jumapili wakati aliposhinda wajumbe wote tisa katika
kisiwa cha Kaskazini cha Mariana.
Chanzo bbc
swahili
No comments:
Post a Comment