Tuesday, 20 March 2018

Trump apendekeza adhabu ya kifo dhidi ya walanguzi wa mihadarati

Rais Donald Trump amesema kuwa anataka kuweka adhabu kali ikiwemo adhabu ya kifo kwa wale watakaobaninika kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Katika hotuba yake aliyoitoa akiwa New Hampshire,wauzaji wa dawa za kulevya wamesababisha vifo vya maelfu ya watu, lakini cha ajabu baada ya kuhukumiwa kufungwa wanakaa muda mfupi tu gerezani jambo ambalo anasema haliridhishwi nalo.
Ameongeza kuwa tatizo hili linaweza kuondolewa kwa kutumia akili na kuwa imara pamoja na kutenga fedha.
Hata hivyo Rais Trump ameelezea mikakati iliyowekwa tayari katika kukabilianba na dawa za kulevya hadi sasa.
Rais Trump ameahidi kujenga taifa huru katika masuala ya matumizi ya dawa za kulevya kwa kizazi kijacho na kuhakikisha hakuna mazingira yatakayosababisha watu kujitumbukiza katika matumizi ya kulevya
chanzo BBC


No comments:

Post a Comment