Vikosi vya maafisa wa usalama nchini Ubelgiji vinawasaka watu wawili baada ya maafisa wa polisi kufyatuliwa risasi katika oparesheni dhidi ya ugaidi katika mji mkuu wa Brussels.
Kisa hicho kilitokea katika makaazi ya kusini ya Forest.Maafisa watatu walijeruhiwa huku mmoja wao akijeruhiwa vibaya.
Mwendesha
mashtaka amesema kuwa uvamizi huo unahusishwa na shambulio la Paris ambalo
liliwaua watu 130 mwezi Novemba.
Maafisa wa
polisi wa Ubelgiji wamekuwa wakijaribu kuwasaka wapiganaji kutoka kwa kundi la
Islamic State.
Baada ya kisa
cha Jumaane ,maafisa wa polisi wamesema kuwa wanawasaka washukiwa wawili
waliotorokea kwenye paa la nyumba.
Eric Van Der
Sypt,msemaji wa waendesha mashataka hao waliambia AFP kwamba maafisa wa polisi
walifyatuliwa risasi wakati wa shambulio hilo la jumanne mchana.
Ameongezea kuwa
msako huo unahusishwa na uchunguzi wa shambulio la Paris.
Chanzo bbc swahili
No comments:
Post a Comment