Imekuwa siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa
mwanzilishi wa taifa la Korea Kaskazini Kim Il-sung
|
Korea
Kaskazini imefanya jaribio la kufyatua kombora katika pwani yake ya mashariki,
lakini dalili zinaonesha jaribio hilo halikufanikiwa, maafisa wa Marekani na Korea
Kusini wanasema.
Bado
haijabainika roketi iliyotumiwa ilikuwa ya aina gani lakini inadhaniwa
majaribio hayo yalikuwa ya kombora la masafa la wastani kwa jina “Musudan”
ambalo taifa hilo lilikuwa halijalifanyia majaribio.
Shughuli
hiyo ilikuwa ikifanyika siku ambayo ni ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa
mwanzilishi wa taifa la Korea Kaskazini Kim Il-sung.
Imetokea
huku hali ya wasiwasi ikiwa imetanda rasi ya Korea.
Shirika
la habari la Korea Kusini Yonhap, likinukuu duru za serikali, limesema kombora hilo
lilikuwa aina ya kombora la Musudan, ambalo kitaalamu hujulikana kama BM-25.
Majuzi,
wanajeshi wa Korea Kaskazini walionekana wakisafirisha makombora mawili ya aina
hiyo.
Shirika
hilo limesema habari hizo zikithibitishwa, basi itakuwa mara ya kwanza kwa
Korea Kaskazini kufanyia majaribio makombora ya Musudan, na huenda ikawa na
makombora 50 zaidi.
Jina
Musudan linatokana na kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Korea Kaskazini
ambapo kituo cha kurushia makombora hayo kimejengwa.
Makombora
hayo yanaweza kufika umbali wa kilomita 3,000 na kufikia kambi ya majeshi ya
Marekani iliyopo kisiwa cha Guam katika bahari ya Pasifiki. Hata hivyo hayawezi
kufika Marekani bara.
Rais Kim Jong Un amekuwa akitishia Korea Kusini
na Marekani
Marekani
imesema imekuwa ikifuatilia jaribio hilo la kurusha kombora, lakini bado
haijaweza kuthibitisha habari zaidi.
Korea
Kaskazini, chini ya kiongozi wake wa sasa Kim Jong-un, imekuwa ikitishia
kushambulia Marekani na Korea Kaskazini tangu kuwekewa vikwazo na Umoja wa
Mataifa kwa kufanya jaribio la nne la makombora ya nyuklia.
Siku ya
kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Korea Kaskazini, babu yake Kim, huwa muhimu sana
kwa taifa hilo. Miaka minne iliyopita, Korea Kaskazini ilijaribu kusherehekea
kwa kuzindua kombora lakini juhudi hizo zikafeli.
Chanzo bbc swahili
No comments:
Post a Comment