Monday, 7 March 2016

watu 300,000 waadhibiwa kwa ufisadi china

Na Neema Dandida


 
 
 
 
Rais xi ameangazia sana vita dhidi ya ulaji rushwa
Chama tawala cha Kikomunisti nchini Uchina kimesema maafisa karibu 300,000 wa chama hicho waliadhibiwa mwaka jana kwa tuhuma za ufisadi.
MatangazoMaafisa 200,000 walipewa kilichodaiwa kuwa “adhabu ndogo” huku wengine 80,000 wakipewa adhabu kali.
Rais Xi Jinping amefanya vita dhidi ya ufisadi kuwa ajenda kuu ya utawala wake.

Maafisa wakuu wa kisiasa wamefungwa jela baada ya kupatikana na makosa ya ufisadi.

Kila siku, ni kama kawaida kupata habari za maafisa wa serikali waliochunguzwa au kuadhibiwa kwa sababu ya ufisadi, kutumia vibaya mamlaka au tuhuma nyingine zinazohusiana na ulaji rushwa.

Idadi ya walioadhibiwa mwaka 2015 ilitangazwa wakati wa kikao cha kila mwaka cha bunge la Uchina.
chanzo bbc swahili

No comments:

Post a Comment