Kamishna wa
Jumuiya ya Ulaya wa maswala ya wahamiaji amesema kuwa Ugiriki imefurika na
wakimbizi na wahamiaji.
Dimitris
Avramopolous ametoa wito kwa wanachama wote wa jumuiya hiyo ya Ulaya kusaidia
katika kusuluhisha hali hiyo badala ya kuiachia Ugiriki au Italia pekee.
Kati ya
wahamiaji 2003 wanakisiwa kuingia Ugiriki kila siku.
Wengi wao
hawawezi kusonga mbele kwa sababu ya vikwazo vikali vilivyowekwa na Austria na
mataifa ya Balkan.hamiaji wanaoingia Ugiriki
Mwandishi wa BBC
anasema kuwa matamshi ya Bwana Avromopolous ni ishara kuwa kiongozi huyo wa
wahamiaji katika Jumuiya hana nia ya taifa lake kuzuiliwa kuwa mwanachama wa
muungano wa paspoti wa Schengen.
Kwa kawaida mtu
ye yote aliye na paspoti ya Schengen ana uhuru wa kusafiri bila vikwazo kwa
mataifa mengine wanachama wa muungano huo.
chanzo bbc swahili
No comments:
Post a Comment