Na Neema Dandida
Korea Kaskazini ilifanyia majaribio bomu la
haidrojeni Januari mwaka huu.
Korea
Kusini imesema imepata dalili kwamba Korea Kaskazini inajiandaa kufanya jaribio
la tano la bomu la nyuklia, Rais Park Geun-hye amesema.
Hakufafanua
zaidi kuhusu dalili hizo, lakini ameagiza jeshi la nchi yake kuwa tayari,
shirika la habari la nchi hiyo limesema.
Kumekuwa
na ripoti katika vyombo vya habari nchini Korea Kusini kwamba kumeongezeka
shughuli katika kituo cha majaribio ya silaha za nyuklia cha Korea Kaskazini
cha Punggye-ri, ambapo majaribio ya awali yalitekelezwa.
Iwapo
Pyongyang itaendelea na kufanyia majaribio bomu la nyuklia, basi itakuwa ni
kukaidi zaidi vikwazo vikali ilivyoongezewa na Umoja wa Mataifa mwezi jana.
"Tupo
katika hali ya kutatanisha, hatujui iwapo Korea Kaskazini inaweza kufanya
uchokozi kama njia ya kujitetea kutokana na kutengwa na jamii ya kimataifa na
pia kuimarisha uungwaji mkono ndani ya nchi,” Bi Park aliambia maafisa wake
wakuu wa jeshi, shirika la habari la Yonhap liliripoti.
Mwezi
Januari, Korea Kaskazini ilifanya jaribio la nne la silaha za nyuklia na
baadaye ikarusha kombora baharini.
Hatua
hiyo iliongeza hali ya wasiwasi katika rasi ya Korea.
Waangalizi
wanasema huenda jaribio hilo la bomu likafanywa kabla ya mkutano mkuu wa chama
tawala cha Workers' Party mjini Pyongyang mwezi Mei.
Wataalamu
wanaamini Korea Kaskazini haina uwezo wa kiteknolojia wa kuweka silaha ya
nyuklia kwenye kombora, ingawa imepiga hatua kubwa katika mpango wake wa
nyuklia miaka ya karibuni.
chanzo bbc swahili
No comments:
Post a Comment