Na Neema Dandida
Maelfu ya wahamiaji kutoka Afrika na
Mashariki ya Kati wamekuwa wakijaribu kufika Ulaya.
Wahamiaji
karibu 400, wengi wao kutoka Somalia, wanahofiwa kuzama katika bahari ya
Mediterranean wakijaribu kuelekea bara Ulaya.
Taarifa
kutoka Misri zinasema wahamiaji hao walikuwa wakitumia boti nne kusafiri.
Jamaa za
baadhi ya wahamiaji hao wamesema baadhi ya wahamiaji waliokolewa na kikosi cha
wana maji kutoka Ugiriki na sasa wamo Ugiriki.
Balozi wa
Somalia nchini Misri amethibitisha kisa hicho lakini akasema bado wanatafuta
maelezo zaidi.
chanzo bbc swahili
No comments:
Post a Comment