Dartmouth
College Louisa HowardSPL
Shirika
la madaktari wasio na mipaka limesema robo tatu ya watu wazima wenye maambukizi
ya virusi vya Ukimwi Magharibi na Afrika ya kati wapo katika mazingira
yasiyowaruhusu kupata Matibabu.
Pamoja na
idadi hiyo kubwa ya watu wazima wasio katika mazingira rafiki kwa
matibabu,shirika hilo la Medecins Sans Frontieres linasema asilimia 90 pia ya
watoto wadogo wenye maambukizi ya virusi hivyo vya Ukimwi wanakabiliana na
vikwazo kupata huduma za kiafya
MSF limesisitiza
kuwa kama hakutakuwa na jitihada za makusudi kuhakikisha huduma za afya kwa
waathirika hao zinafika Afrika Magharibi na kati na vinginevyo,malengo
kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo ifikapo 2020 hayatafanikiwa.
Ripoti
hiyo imeleza kuwa takribani watu milioni tano katika ukanda wa Afrika hawapati
dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi,ambapo zaidi ya
asilimia 20 ya watu wana maambukizi ya virusi katika eneo hilo,huku nusu tu
ndiyo wanaoweza kufikiwa na matibabu.
Hata
hivyo takwimu za shirika hilo zinaonyesha kuwa idadi ya watu wenye maambukizi
ya virusi vya ukimwi Afrika Magharibi na kati ni ndogo ikilinganishwa nchi za
kusini mwa Afrika ambapo nusu ya idadi ya watu wote wanamaabukizi na nusu yao
pia wapo katika mazingira mazuri kupatiwa matibabu
chanzo bbc swahili
No comments:
Post a Comment