Rais wa
Marekani,Barack Obama amelaani mauaji yaliyotokea Orlando
|
Rais wa Marekani,Barack Obama amesema shambulio la
risasi katika Klabu ya usiku mjini Orlando ni la kigaidi na ni kitendo cha
chuki
Takriban watu 50 wamepoteza maisha na wengine 53
wamejeruhiwa siku ya Jumapili, baada ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha
kufyatulia risasi Klabu moja ya usiku iliyokuwa ikiwakutanisha watu wa mapenzi
ya jinsia moja mjini Orlando nchini Marekani.
Polisi nchini humo wamesema kuwa ni shambulio baya halikuwahi
kutokea katika historia ya nchi hiyo.
Rais Obama amesema Marekani inaungana ikiwa na
huzuni,mshtuko mkubwa na inalenga kutetea watu wake, pia amesema mauaji hayo
yanawakumbusha ni namna gani ilivyo rahisi kupata silaha hatari nchini
Marekani.
Shirika la kijasusi nchini humo,FBI limemtambua
mshambuliaji huyo kuwa raia wa Marekani,Omar Mateen ambaye naye aliuawa wakati
wa mapambano na vikosi vya usalama katika klabu hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya
watu 300 ndani yake.
chanzo bbc swahili
No comments:
Post a Comment