Na Neema Dandida
Harakati ya Vijana wa Bunia katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo imewataka viongozi wa serikali kuchukua hatua za lazima
kwa ajili ya kuimarisha usalama katika mji huo wa kaskazini mashariki mwa nchi
hiyo.
Harakati hiyo ya vijana wa mji wa Bunia ambao ni makao makuu ya mkoa wa
Ituri ulioko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
imebainisha katika taarifa yake kwamba, maafisa wa setrikali katika mji huo
wanapasawa kuchukua hatua za lazima kwa ajili ya kuimarisha usalama wa raia na
mali zao katika mji huo.
Harakati hiyo imesisitiza kwamba, kumetokea mashambulio ya silaha katika
siku za hivi karibuni katika maeneo tofauti ya Bunia pamoja na viunga vya mji
huo. Silvain Agernowoth, Mratibu wa Harakati ya Vijana wa Bunia amewaambia
waandishi wa habari kwamba, raia wa mji huo siku ya Jumamosi na Jumapili za
wiki iliyopita walifanikiwa kuzima hujuma na mashambulio saba pasina ya
uingiliaji wa polisi.
Uwanja wa ndege wa Bunia
Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaamini kuwa, kutokuwa na
uwezo jeshi la nchi hiyo na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataigfa nchini
humo MONUSCO wa kuyatokomeza makundi ya waasi ni jambo ambalo limechangia kwa
sehemu kubwa kuenea ukosefu wa usalama na amani katika maeneo ya mashariki mwa
nchi hiyo.
Eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limekuwa
likishuhudia machafuko kwa zaidi ya miaka 20 sasa kutokana na kuwa ngome ya
makundi kadhaa ya waasi kutoka nchi jirani za Rwanda na Uganda.
Baadhi ya vijiji vya mashariki mwa nchi hiyo vinadhibitiwa na makundi ya
waasi hali ambayo imewafanya wakazi wake kuyaacha makazi yao na kuwa wakimbizi.
Chanzo pars today
No comments:
Post a Comment