Na Neema Dandida
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mamia ya maelfu
ya watoto nchini Nigeria wanakabiliwa na hatari ya ukame.
Peter Lundberg, Mratibu wa muda wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa
Mataifa nchini Nigeria ametahadharisha katika taarifa yake kwamba, karibu
watoto laki nne nchini Nigeria wanakabiliwa na hatari ya ukame
.
Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, raia wengi wa maeneo
mbalimbali ya Nigeria hawana maji safi na salama ya kunywa huku wakikosoa
huduma muhimu za kiafya na kukosa pia fursaa ya masomo.
Wanamgambo wa Boko Haram
Peter Lundberg, amesema, ili kutekeleza mipango ya misaada ya kibinadamu
nchini Nigeria katika mwaka huu, Umoja wa Mataifa ulitaka nchi wafadhili
zisaidie kiasi cha dola milioni 484, lakini hadi sasa ni theluthi moja tu ya
kiasi hicho ndicho kilichopatikana.
Amesema, endapo Umoja wa Mataifa hautapata kiasi hicho cha fedha kwa
wakati, wananchi wengi wa Nigeria hususan wanawake na watoto wanatakabiliwa na
hatari ya kifo kutokana na tishio la ukame.
Takwimu za Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF zinaonyesha kuwa,
karibu watu milioni moja na laki nne wakiwemo wanawake na watoto wengi katika
nchi za Ukanda wa Ziwa Chad ikiwemo Nigeria wamelazimika kuyakimbia makazi yao
kutokana na vijiji vyao kushambuliwa mara kwa mara na kundi la kigaidi la Boko
Haram.
chanzo pars today
No comments:
Post a Comment