Waziri wa Mafuta wa Nigeria amesema kuwa, uzalishaji mafuta umerejea katika hali yake ya kwaida nchini humo.
Shirika la habari la IRIB
limemnukuu Emmanuel Ibe Kachikwu akisema hayo jana na kuongeza kuwa,
uzalishaji mafuta nchini Nigeria umefikia mapipa milioni mbili na laki moja kwa
siku jambo ambalo linaonesha kufikiwa kiwango chake cha kawaida cha kabla ya
kuharibiwa taasisi za kuzalisha mafuta za nchi hiyo.
Wiki chache zilizopita,
serikali ya Nigeria ilifanya mazungumzo na kundi la waasi wa Niger Delta la
kusini mashariki mwa nchi hiyo kwa upatanishi wa mashirika ya kigeni na jeshi
la polisi kwa lengo la kulitafutia ufumbuzi tatizo la ukosefu wa amani ambalo
limeathibiri vibaya eneo hilo kwa muda mrefu sasa.
Uharibifu wa mabomba ya
mafuta mara nyingi hufanyika kwa lengo la kuiba mafuta hayo, na jambo hilo
limekuwa la kawaida sana nchini Nigeria, ambayo ni mzalishaji mkuu wa mafuta
ghafi barani Afrika.
Waziri wa Mafuta wa Nigeria
amesema, mazungumzo baina ya serikali na waasi yamekuwa na mafanikio makubwa. Amesema,
malengo ya mwaka 2017 ya nchi yake ni kumaliza kabisa vitendo vya uharibifu
vinavyofanywa na makundi mbalimbali ya nchi hiyo.
Sehemu kubwa ya mafuta
ghafi ya Nigeria yanazalishwa katika eneo la Niger Delta la kusini mashariki
mwa nchi hiyo.
Asilimia 80 ya bajeti ya Nigeria inategemea uuzaji nje mafuta ghafi ya nchi hiyo.
Asilimia 80 ya bajeti ya Nigeria inategemea uuzaji nje mafuta ghafi ya nchi hiyo.
chanzo pars today
No comments:
Post a Comment