Sudan, faru pekee wa kiume aina ya Northern White Rhino aliyekuwa amesalia hai duniani, amekufa akiwa na miaka 45. |
Faru huyo alikuwa akitibiwa kwa muda na matabibu katika shamba
kubwa la uhifadhi wa wanyama la kituo hicho kwa muda kutokana na matatizo
yaliyotokana na kuzeeka kwake. Alikuwa na vidonda ambavyo vilikuwa vinakosa kupona kutokana na
umri wake.
Sudan alikuwa maarufu sana duniani na alikuwa nembo ya kutetea
juhudi za kupigana na ujangili na kuwaokoa wanyama walio katika hatari ya
kuangamia.
Alinusurika kuuawa porini alipohamishiwa katika kituo cha kuhifadhi wanyama cha Dvur Kralove miaka ya 1970.
Miaka ya baadaye, alirejeshwa Afrika na kuanza kutunzwa katika
kituo cha Ol Pejeta. Mtandao wa Tinder kutumiwa kuokoa faru
Alichangia kuendeleza faru wa aina yake kwa kutungisha mimba
faru wengine na kuchangia kuzaliwa kwa faru wengine wawili wa aina yake ambao
sasa ndio pekee waliosalia hai. Faru hao kwa jina Najin na Fatu ni wa kike lakini ni tasa.
Matumaini pekee sasa ya kuendeleza faru wa aina ya Northern
White Rhino ni kupitia teknolojia ya kutungisha mbegu kwenye mayai ya mnyama
nje ya mwili wa mnyama huyo, maarufu kama IVF.
|
Chanzo BBC