Na Neema Dandida
Alikamatwa alipokuwa katika makao makuu ya
chama chake cha FDC Ijumaa, siku moja kabla ya kutangazwa kwa matokeo, na
akarejeshwa kwake nyumbani baadaye jioni.
Amekuwa
akikamatwa kila anapojaribu kuondoka nyumbani kwake na kisha kurejeshwa baadaye
jioni.
Polisi wamekuwa wakizingira nyumba yake na kuwazuia watu kuingia.
Chama hicho
kimepinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Jumamosi
ambapo Rais Museveni alitangazwa mshindi.
Mawakili
wake pia wanatafakari uwezekano wa kuwasilisha kesi kortini kupinga matokeo
hayo ya urais.
Bw Besigye
amelalamika vikali kutokana na hatua ya kuzuiliwa nyumbani na maafisa wa
usalama.
Ujumbe
uliopakiwa kwenye ukurasa wake wa Facebook, baada yake kurejeshwa nyumbani
kwake Alhamisi, unasema: “Jioni hii, najihisi kama naweza kuwa ‘gaidi’ halisi.”
Amesema
iwapo kuna sababu ya kumzuilia, basi anafaa kuzuiliwa gerezani au eneo
lililotangazwa kuwa seli la sivyo aachiliwe huru na kuruhusiwa kutembea.
Alhamisi
alikamatwa alipokuwa akijaribu kuelekea afisi za FDC eneo la Najjanankumbi
mwendo wa saa tano mchana na akaachiliwa huru saa tatu usiku.
Chanzo bbc swahili
No comments:
Post a Comment