Shirika
la ndege la British Airways limekubali kulipa fidia kundi la watoto
walionyanyaswa kingono na mmoja wa marubani wake nchi za Afrika Mashariki.
Kiasi
cha fidia hata hivyo hakijafichuliwa.
Simon Wood alidaiwa kuwanyanyasa kingono watoto nchini Tanzania, Kenya na Uganda kati ya mwaka 2003 na 2013 alipokuwa akifanya kazi ya kujitolea.
Ingawa
shirika hilo la ndege limekubali kulipa fidia, halijakubali lawama.
Simon
Wood alijishindia tuzo kutoka kwa British Airways kutokana na kazi zake za
kusaidia wasiojiweza katika jamii katika vituo vya kuwatunza mayatima Afrika
miaka mitatu iliyopita.
Alishtakiwa
kumnyanyasa mtoto nchini Uingereza na akajiua.
wafanyakazi wa British Airways wameonywa kuhusu tabia yake nchini
Kenya mwaka 2004.
Watoto
38, mdogo zaidi akiwa na umri wa miaka minne pekee wakati wa kufanyika kwa
dhuluma hizo, walishtaki shirika hilo la ndege.
British
Airways imesema madai hayo yanatisha na ingawa haijakiri lawama hata kidogo,
imekubali kulipa fidia.
Mawakili
waliowakilisha waathiriwa wamesema waajiri wengine, wanaowatuma wafanyakazi wao
kufanya kazi za kusaidia jamii, wanafaa kuhakikisha hatua zinachukuliwa kuzuia
unyanyasaji.
chanzo Bbc swahili
No comments:
Post a Comment