Aliyekuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam
(DART), Asteria Mlambo (kulia) akitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es
Salaam jana baada ya kusomewa mashtaka yeye na wenzake watatu kwa kuisababishia
Serikali hasara ya Sh milioni 83.5.
Na Neema Dandida
MABOSI
watatu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), akiwemo Mtendaji Mkuu wa
mradi huo, Asteria Mlambo, wamepandishwa kizimbani, kwa tuhuma za kuisababishia
serikali hasara ya Sh milioni 83.5.
Mbali
na Asteria, washitakiwa wengine wanaokabiliwa na mashitaka hayo ya uhujumu
uchumi ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa
mradi huo, Francis Kugesha na Mkurugenzi wa kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe.
Walifikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa
mashitaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage.
Walisomewa
mashitaka na wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),
Jackline Nyantori akisaidiwa na Estazia Wilson na Stellah Mafuru.
Nyantori
alidai kati ya Septemba Mosi na Oktoba Mosi 2013, Kinondoni jijini Dar es Salaam,
Asteria, Katale na Kugesha wakiwa wafanyakazi wa mradi huo, walishindwa
kutekeleza majukumu yao vizuri na kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni
83.5.Katika mashitaka yanayomkabili Mwakatobe, inadaiwa Juni 29, 2005 katika ofisi za kodi Ilala, jijini Dar es Salaam, alitoa taarifa za uongo kwa maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), wakati akiwasilisha taarifa ya fedha ya mwaka 2004 na ya 2005 ya kampuni yake ya Yukan Business, jambo lililosababisha alipe kodi ndogo.
Awali,
Wakili Nyantole alidai kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) amewasilisha hati ya
kuruhusu mahakama hiyo, kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi hivyo
washitakiwa wataruhusiwa kujibu mashitaka yao.
Washitakiwa
walikana mashitaka na upande wa Takukuru ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo
haujakamilika, pia hawana pingamizi ya dhamana kwa washitakiwa.
Hakimu
Mwijage alisema Asteria, Katale na Kugesha watapata dhamana endapo kila mmoja
atakuwa na mdhamini mmoja anayefanyakazi serikalini au kwenye taasisi
inayofahamika, atakayesaini hati ya Sh milioni 15. Pia kila mshitakiwa
awasilishe Sh milioni 15 au hati isiyohamishika yenye thamani ya Sh milioni 15.
Kwa
upande wa Mwakatobe, dhamana yake ipo wazi endapo atapata mdhamini mmoja mwenye
barua kutoka taasisi inayofahamika, asaini hati ya Sh milioni tano.
Wote
waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti. Asteria na Katale wametakiwa
kuwasilisha hati hizo Machi 3 mwaka huu. Kesi itatajwa tena Machi 9 mwaka huu.
chanzo ipp media
No comments:
Post a Comment