Na Neema Dandida
WAZIRI wa Mambo
ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk
Augustine Mahiga amesema Watanzania waliopo nje ya nchi ni zaidi ya milioni
moja na idadi yao inazidi kuongezeka.
Hivyo
wizara inajipanga kuanzisha kitengo maalumu katika nchi hizo kwa ajili ya
kusema na kutetea nchi nje ya nchi kama wafanyavyo nchi nyingine.
Alisema
kuna Watanzania wengi nje ya nchi na wanazidi kuongezeka lakini kwa bahati
nzuri Watanzania hao siyo wakimbizi na hakuna aliyezama baharini, bali wengi
wanaenda kutafuta maisha kwa kutumia njia halali.
Balozi
Mahiga alisema nchi nyingi alizokuwepo wapo hawana vibali, lakini wanatafuta na
idadi inaongezeka na wizarani hapo kuna idara maalumu ya kuwashughulikia.
Pia
alisema kwa muundo wa wizara mbili kuwa moja iliyopo sasa wataangalia
wakurugenzi walio muhimu na wasio muhimu kupewa kazi nyingine.
Akizungumzia
migogoro iliyopo baina ya Rwanda na Burundi, alisema Tanzania imekuwa mstari wa
mbele kuishughulikia na mara nyingi amekwenda katika nchi hizo kwa lengo la
kutafuta muafaka.
Alisema
nchi imekuwa ikifanya hivyo kutokana na kuwa nchi hizo ni majirani hivyo
kuathirika kwao ni kuadhirika kwa ukanda mzima na pia kuwa Tanzania ni
Mwenyekiti wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na hivi karibuni watakuwa na
kikao cha kuendelea na mazungumzo ya amani.
chanzo ipp media
No comments:
Post a Comment