Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amemsimamisha kazi jaji Philip Tunoi wa mahakama kuu kwa tuhuma za kupokea rushwa ya dola milioni 2.
Rais Kenyatta pia ameteua
jopo la watu saba kuchunguza tuhuma hizo, kuwa alipokea rushwa hiyo ili atoe
upendeleo kwa Gavana wa Nairobi Bw Evans Kidero wakati wa kesi ya kuwekewa
pingamizi na wabunge, Agosti 2014.
Awali ikulu ya Nairobi
ilisema Rais hataandaa jopo la uchunguzi kwa kuwa jaji Tunoi aliomba kustaafu,
lakini wataalamu wa Sheria walisema kama Rais asingechukua hatua hiyo ndani ya
wiki mbili zilizoishia jana tangu kuwasilishwa kwa tuhuma, basi angekuwa
anakiuka katiba
chanzo radio international
No comments:
Post a Comment