Rais John Magufuli akizungumza na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dk Richard Sezibera Ikulu |
Dar es Salaam.
RAIS
John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki, Dk Richard Sezibera Ikulu Dar es Salaam.
Pamoja
na mambo mengine, Rais Magufuli amepokea taarifa ya maandalizi ya Mkutano wa
Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Machi 2, mwaka huu
mjini Arusha.
Rais
Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha
nchi tano wanachama ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Akizungumza
baada ya mazungumzo hayo, Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo, Dk Sezibera amesema
maandalizi kuhusu mkutano huo yanakwenda vizuri.
Amesema
pamoja na mambo mengine mkutano huo, utajadili masuala kadhaa yakiwemo mpango
wa kuanzisha viwanda vya magari ndani ya Jumuiya ili kupunguza uingizaji wa
magari kutoka nje ya nchi na Marais kuzindua pasi ya kusafiria ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Kuhusu
hali ya Jumuiya, Dk Sezibera amesema inaendelea vizuri na alitaja baadhi ya
mambo yaliyofanyika kuwa ni kutiwa saini kwa mkataba wa umoja wa forodha,
makubaliano ya soko la pamoja na makubaliano ya sarafu moja.
Mengine
ni kuwepo kwa mazungumzo kuhusu uimarishaji wa miundombinu kama vile reli na
umeme ndani ya Jumuiya, na mazungumzo kuhusu umoja wa kisiasa.
chanzo ippmedia
No comments:
Post a Comment