mmoja wa watoto wakiwa katika hospitali nchini Brazili akiwa na mzazi wake baada ya uchunguzi juu ya ugonjwa wa Zika

NaNeema Dandida     

Wanasayansi kutoka kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa CDC nchini Marekani wameanza kufanya utafiti nchini Brazil ili kujua uhusiano kati ya Virusi vya Zika na watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo.
Timu za wanasayansi zimekuwepo katika jimbo la Paraeeba, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, jimbo ambalo limeathirika zaidi na Virusi.

Timu nane zinazoundwa na cdc na mawakala wa maswala ya afya walienda kwenye maeneo yaliyoathirika na kuchukua sampuli ya damu na kuwahoji wamama walioathirika na wamama ambao watoto wao walizaliwa wakiwa na vichwa vidogo.
Katika kipindi cha majuma yajayo, watakusanya taarifa kutoka kwa mamia ya wamama katika jimbo la Paraeeba, jimbo la pili lililoathirika zaidi.

Katika Ripoti ya  Wizara wa Afya wa Brazil imethibitisha watoto 587 wana vichwa vidogo asilimia 75 zaidi ya wiki iliyopita huku maelfu ya watoto wanachunguzwa.

Baada ya kutangazwa hali ya taadhari ya kiafya, Rais wa Shirika la Afya duniani, Margaret Chan aliwasili Brasilia kufuatilia hali ilivyo.

Akiwa huko alikutana Rais wa Brazil,Dilma Roussef amesema kuwa anafurahishwa na namna Serikali inavyoshughulikia tatizo hilo na kutaka jamii isaidiwe kupambana na mbu anayeeneza virusi vya Zika.
     
  chanzo bbc swahili