Friday, 4 March 2016

Trump akabiliwa mdahalo wa Republican



Na Neema Dandida
Wagombea wakuu Republican sasa wamebaki wane


 
 
 
 
Mgombea urais Donald Trump ameshambuliwa sana na wagombea wenzake katika mdahalo wa chama cha Republican, muda mfupi baada ya wanasiasa wakongwe wa chama hicho kuwahimiza wapiga kura wasimuunge mkono.
Bw Trump, anayeongoza kwenye kura za maoni kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea wa urais wa chama cha Republican, amelazimika kujitetea vikali dhidi ya shutuma kutoka kwa Marco Rubio na Ted Cruz.
Katika mdahalo huo uliofanyika Detroit, Bw Trump amekiri kwamba amebadilisha msimamo wake mkali lakini akasema kwamba kuweza kubadilika ni nguvu na si udhaifu. 
Baadhi ya wanachama wakuu wa Republican wanasema Bw Trump hafai na kwamba hawezi kushinda urais dhidi ya chama cha Democratic.
Mdahalo huo ulioandaliwa na kituo cha Fox News ulianza kwa Bw Trump kuulizwa kuhusu shutuma za awali kutoka kwa Mitt Romney, aliyewania urais 2012, aliyesema mfanyabiashara huyo ni mchokozi, mlafi na aliyejaa chuki.
Trump na Mitt Romney awali

 

 
 
 
 
 
Bw Trump amempuuzilia mbali Romney na kumtaja kuwa “mgombea aliyefeli”. Lakini mara moja alijipata akishambuliwa na Bw Rubio.
Seneta huyo wa Florida alisema hatasalimisha vuguvugu la wahafidhina kwa mtu anayedhani “nuclear triad” (mkusanyiko wa silaha za nyuklia) ni bendi ya rock kutoka miaka ya 1980.
chanzo: Bbc Swahili


1 comment: