marco Rubio na Ronald trump katika mjadala |
Mgombea
wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Marco Rubio amemshtumu Donald
Trump kwa kusema kuwa Uislamu unachukia Marekani katika mjadala uliokuwa moja
kwa moja runingani.
Bwana
Rubio ambaye anakabiliwa na ushindani wa maisha yake katika jimbo la Florida
siku ya Jumanne amesema kuwa Uislamu una tatizo la itikadi kali lakini
akaongezea kuwa Waislamu wengi wanapenda Wamerekani.
''Marais
hawawezi kusema kile wanachotaka ,kuna madhara'',alisema huku raia wakimpigia
makofi.Wagombea hao wanne wa chama cha Republican walisikia maombi kutoka kwa viongozi wa chama hicho kuwa na mjadala wa amani.
Ikilinganishwa na mjadala uliopita ambao ulikabiliwa na na matusi ya kibinafsi mjadala huu ulikuwa na muongozo mzuri huku wagombea wote wakitoa malengo ya sera zao.
''Kufikia sasa siamini vile tumekuwa watulivu hapa'',bwana Trump alinukuliwa akisema.
Lakini katika swala la Uislamu,kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Trump na wagombea wengine huku wenzake wote wakitofautiana naye kwamba familia za magaidi ziangamizwe.
chanzo bbc swahili
No comments:
Post a Comment