Friday, 11 March 2016

walio na hofu ya wahamiaji sio wabaguzi

Na Neema Dandida


askofu mkuu Justin welby
Askofu mkuu wa kanisa la Cantebury Justin Welby amesema kuwa ni makosa kuwataja watu walio na wasiwasi kuhusu uhamiaji kuwa wabaguzi.
Kuna wasiwasi kuhusu athari za nyumba za kuishi ,kazi na afya,aliliambia bunge.
Hatahivyo aliitaka Uingereza kuchukua baadhi ya wahamiaji na wakimbizi.
Bwana Welby pia alitaka kufanyika kwa mjadala ulio na maono kuhusu kura ya maoni na kusema kuwa hakuna mkristo yeyote aliye na maoni ya sawa kuhusu vile Waingereza wanapaswa kupiga kura.
Amesema:Lazima tujiamulie lakini pia lazima tujue tunafanya nini duniani.Taifa hili lina historia ya kipekee tukiangazia miaka 100 iliopita.

chanzo bbc swahili

No comments:

Post a Comment