Wednesday, 2 November 2016

Rais Mugabe Aidhinisha 'sarafu mpya' Zimbabwe

 Na Neema Dandida
 
Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametumia mamlaka ya ofisi yake kutoa dikrii inayoidhinisha matumizi ya sarafu mpya nchini humo, licha ya asasi za kiraia kusisitiza kuwa uamuzi huo ni kinyume cha sheria.
Patrick Chinamasa, Waziri wa Fedha wa Zimbabwe amesema Mugabe ametumia kifungu cha 133 cha Sheria ya Mamlaka ya Rais ya 2016, kuidhinisha matumizi ya sarafu hiyo inayoshabihiana na Dola ya Marekani na kufafanua kuwa, kwa sasa ni halali kutumia sarafu hiyo katika mabadilishano ya bidhaa na huduma mbalimbali.
  
Patrick Chinamasa, Waziri wa Fedha wa Zimbabwe.
Hata hivyo aliyekuwa Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, Tendai Biti, amekosoa uamuzi huo wa Mugabe na kusema kuwa ni wa kidikteta na unaokiuka katiba ya nchi.

Nchi ya Zimbabwe imekuwa ikikabiliwa na changamoto za kifedha hasa baada ya kushuka thamani ya sarafu yake kuanzia mwaka 2009 na kuamua kuanza kutumia Dola ya Marekani.
Tangu kipindi hicho, mbali na Dola ya Marekani, raia wa Zimbabwe wamekuwa wakitumia sarafu zingine za kigeni kama Yuro, Yuan ya China, Pauni ya Uingereza na Rand ya Afrika Kusini.

  Maandamano dhidi ya serikali nchini Zimbabwe.

Katika siku za hivi karibuni, Zimbabwe imekuwa ikishuhudia maandamano ya wapinzani wanaomtaka Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 92 aondoke madarakani wakisisitiza kuwa ameshindwa kutatua matatizo ya kiuchumi na ukosefu wa ajira nchini humo.
                                 Chanzo Pars Taday

Rouhani: Uingiliaji wa kigeni umeleta mgawanyiko Mashariki ya Kati


 Na Neema Dandida
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema matatizo yanayolikabili eneo hili la Mashariki ya Kati yamesababishwa na uingiliaji unaofanywa na nchi za kigeni katika masuala ya ndani ya nchi za eneo hilo.
Katika mazungumzo yake na Demetris Syllouris, Rais wa Bunge la Cyprus hapo jana mjini Tehran, Rais Rouhani alisema, ili kuwa na mustakbali wenye mwangaza, maendeleo, usalama na ututivu, nchi za eneo hili sharti zishirikiane na kila moja itekeleze wajibu wake wa kimataifa.
Rais Hassan Rouhani ameelezea kusikitishwa kwake na namna mamilioni ya watu wasio na hatia katika nchi za Iraq, Syria, Yemen na Libya wanavyoendelea kukabiliwa na matatizo chungunzima kutokana na migawanyiko, uhasama na mapigano yaliyochochewa na nchi za Magharibi.


Mazungumzo ya Rais Hassan Rouhani na Demetris Syllouris, Rais wa Bunge la Cyprus Tehran
Kwengineko katika mazungumzo hayo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa uhusiano kati ya Tehran na Nicosia na kubainisha kuwa, ushirikiano huo unaweza kuwa daraja ya kuunganisha Mashariki ya Kati na bara Ulaya pamoja na bara Afrika.
Kwa upande wake, Demetris Syllouris, Rais wa Bunge la Cyprus amesema kuchukuliwa hatua za kijeshi katika kuitafutia ufumbuzi migogoro inayolikabili eneo la Mashariki ya Kati, hakujakuwa na natija nyingine ghairi ya kuzidisha mizozo hiyo na kuibua mingine mipya. Amesema kuwa Cyprus iko tayari kuimarisha uhusiano wa pande mbili na Iran katika nyuga za biashara, uchumi na utamaduni.
Rais wa Bunge la Cyprus ambaye aliwasili nchini Jumapili iliyopita kufuatia mwaliko wa Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu, Ali Larijani, amekutana na kufanya mazungumzo na maafisa mbalimbali wa ngazi za juu wa serikali ya Tehran akiwemo Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
Chanzo Pars Today

Sunday, 12 June 2016

Rais Obama alaani mauaji ya Orlando



Rais wa Marekani,Barack Obama amelaani mauaji yaliyotokea Orlando













Rais wa Marekani,Barack Obama amesema shambulio la risasi katika Klabu ya usiku mjini Orlando ni la kigaidi na ni kitendo cha chuki

Takriban watu 50 wamepoteza maisha na wengine 53 wamejeruhiwa siku ya Jumapili, baada ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha kufyatulia risasi Klabu moja ya usiku iliyokuwa ikiwakutanisha watu wa mapenzi ya jinsia moja mjini Orlando nchini Marekani.

Polisi nchini humo wamesema kuwa ni shambulio baya halikuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.

Rais Obama amesema Marekani inaungana ikiwa na huzuni,mshtuko mkubwa na inalenga kutetea watu wake, pia amesema mauaji hayo yanawakumbusha ni namna gani ilivyo rahisi kupata silaha hatari nchini Marekani.

Shirika la kijasusi nchini humo,FBI limemtambua mshambuliaji huyo kuwa raia wa Marekani,Omar Mateen ambaye naye aliuawa wakati wa mapambano na vikosi vya usalama katika klabu hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya watu 300 ndani yake.

              chanzo bbc swahili

Thursday, 21 April 2016

Maambukizi ya HIV tishio Afrika

Na Neema Dandida
                                      Dartmouth College Louisa HowardSPL 

Shirika la madaktari wasio na mipaka limesema robo tatu ya watu wazima wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi Magharibi na Afrika ya kati wapo katika mazingira yasiyowaruhusu kupata Matibabu.

Pamoja na idadi hiyo kubwa ya watu wazima wasio katika mazingira rafiki kwa matibabu,shirika hilo la Medecins Sans Frontieres linasema asilimia 90 pia ya watoto wadogo wenye maambukizi ya virusi hivyo vya Ukimwi wanakabiliana na vikwazo kupata huduma za kiafya

MSF limesisitiza kuwa kama hakutakuwa na jitihada za makusudi kuhakikisha huduma za afya kwa waathirika hao zinafika Afrika Magharibi na kati na vinginevyo,malengo kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo ifikapo 2020 hayatafanikiwa.

Ripoti hiyo imeleza kuwa takribani watu milioni tano katika ukanda wa Afrika hawapati dawa za kupunguza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi,ambapo zaidi ya asilimia 20 ya watu wana maambukizi ya virusi katika eneo hilo,huku nusu tu ndiyo wanaoweza kufikiwa na matibabu.

Hata hivyo takwimu za shirika hilo zinaonyesha kuwa idadi ya watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi Afrika Magharibi na kati ni ndogo ikilinganishwa nchi za kusini mwa Afrika ambapo nusu ya idadi ya watu wote wanamaabukizi na nusu yao pia wapo katika mazingira mazuri kupatiwa matibabu
 chanzo bbc swahili

Vurugu zaendelea nchini Zambia


Na Neema Dandida
Polisi nchini Zambia wamesema watu wawili wamechomwa moto mjini Lusaka katika vurugu ya ubaguzi wa wenyeji dhidi ya wageni.

Watu Zaidi ya mia mbili na hamsini wamekamatwa baada ya maduka mengi yanayomilikiwa na wanyaruanda kuvamiwa.Uvamizi huo ulitokea baada ya wanyaruanda kushutumiwa kuua watu na kutumia viungo vyao kuvutia wateja.

o Padre Charles Chilinda ameiambia BBC kuwa kanisa lake linafanya jitihada zote ili kuweza kuwasaidia wahanga ambao wamekwenda kuomba hifadhi kanisani.

"Kitu ambacho tunaweza kuwapa ni kwamba watakuwa na usalama wa kutosha kuwa hapo,tutaenda kuwaangalia na kuwaeleza kuwa hawa sio wazambia ambao wanagombana nao.hali hii haikubaliki ,kila mtu aliyepo katika ardhi ya Zambia analindwa na katiba ya Zambia.

Ni jukumu letu kudumisha Amani na tushirikiane katika kulitokomeza hili"
chanzo bbc swahili

Kenya yailaumu Tanzania kuhusu raia wa Ethiopia


Ramani ya mpaka wa Kenya na Tanzania

Kenya imeilaumu Tanzania kwa kuwaweka raia wa Ethiopia katika eneo lake la mpaka siku ya Jumanne badala ya kuwarudisha makwao kulingana na ripoti ya gazeti la The standard nchini Kenya.

Raia hao wa Ethiopia walikuwa wamewachiliwa huru baada ya kuhudumia vifungo vya mashtaka tofauti ya uhalifu nchini Tanzania.

Maafisa wa polisi wameagizwa kutowaruhusu wageni hao kuingia nchini Kenya.''Watarudishwa nchini Tanzania walikotoka.

Kisa hicho hakikubaliki na hakiruhusiwi na sheria'',Afisa wa Kenya Henry Wafula alinukuliwa akisema.
chanzo bbc swahili