Wednesday, 2 November 2016

Serikali ya DRC yatakiwa kuimarisha usalama katika mji wa Bunia

Na Neema  Dandida
 
Harakati ya Vijana wa Bunia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewataka viongozi wa serikali kuchukua hatua za lazima kwa ajili ya kuimarisha usalama katika mji huo wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Harakati hiyo ya vijana wa mji wa Bunia ambao ni makao makuu ya mkoa wa Ituri ulioko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imebainisha katika taarifa yake kwamba, maafisa wa setrikali katika mji huo wanapasawa kuchukua hatua za lazima kwa ajili ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao katika mji huo.

Harakati hiyo imesisitiza kwamba, kumetokea mashambulio ya silaha katika siku za hivi karibuni katika maeneo tofauti ya Bunia pamoja na viunga vya mji huo. Silvain Agernowoth, Mratibu wa Harakati ya Vijana wa Bunia amewaambia waandishi wa habari kwamba, raia wa mji huo siku ya Jumamosi na Jumapili za wiki iliyopita walifanikiwa kuzima hujuma na mashambulio saba pasina ya uingiliaji wa polisi.
 
Uwanja wa ndege wa Bunia 

Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaamini kuwa, kutokuwa na uwezo jeshi la nchi hiyo na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataigfa nchini humo MONUSCO wa kuyatokomeza makundi ya waasi ni jambo ambalo limechangia kwa sehemu kubwa kuenea ukosefu wa usalama na amani katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo.

Eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limekuwa likishuhudia machafuko kwa zaidi ya miaka 20 sasa kutokana na kuwa ngome ya makundi kadhaa ya waasi kutoka nchi jirani za Rwanda na Uganda.

Baadhi ya vijiji vya mashariki mwa nchi hiyo vinadhibitiwa na makundi ya waasi hali ambayo imewafanya wakazi wake kuyaacha makazi yao na kuwa wakimbizi.
Chanzo pars today

Umoja wa Mataifa: Mamia ya maelfu ya watoto wa Nigeria wanakabiliwa na hatari ya ukame

Na Neema Dandida

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mamia ya maelfu ya watoto nchini Nigeria wanakabiliwa na hatari ya ukame.
 Peter Lundberg, Mratibu wa muda wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Nigeria ametahadharisha katika taarifa yake kwamba, karibu watoto laki nne nchini Nigeria wanakabiliwa na hatari ya ukame
.
Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, raia wengi wa maeneo mbalimbali ya Nigeria hawana maji safi na salama ya kunywa huku wakikosoa huduma muhimu za kiafya na kukosa pia fursaa ya masomo.

Wanamgambo wa Boko Haram
Peter Lundberg, amesema, ili kutekeleza mipango ya misaada ya kibinadamu nchini Nigeria katika mwaka huu, Umoja wa Mataifa ulitaka nchi wafadhili zisaidie kiasi cha dola milioni 484, lakini hadi sasa ni theluthi moja tu ya kiasi hicho ndicho kilichopatikana.

Amesema, endapo Umoja wa Mataifa hautapata kiasi hicho cha fedha kwa wakati, wananchi wengi wa Nigeria hususan wanawake na watoto wanatakabiliwa na hatari ya kifo kutokana na tishio la ukame.
Takwimu za Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF zinaonyesha kuwa, karibu watu milioni moja na laki nne wakiwemo wanawake na watoto wengi katika nchi za Ukanda wa Ziwa Chad ikiwemo Nigeria wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na vijiji vyao kushambuliwa mara kwa mara na kundi la kigaidi la Boko Haram.
                                chanzo pars today

Uzalishaji mafuta warejea katika hali yake ya kawaida nchini Nigeria

Na Neema Dandida
Waziri wa Mafuta wa Nigeria amesema kuwa, uzalishaji mafuta umerejea katika hali yake ya kwaida nchini humo.

Shirika la habari la IRIB limemnukuu Emmanuel Ibe Kachikwu akisema hayo jana na kuongeza kuwa, uzalishaji mafuta nchini Nigeria umefikia mapipa milioni mbili na laki moja kwa siku jambo ambalo linaonesha kufikiwa kiwango chake cha kawaida cha kabla ya kuharibiwa taasisi za kuzalisha mafuta za nchi hiyo.

Wiki chache zilizopita, serikali ya Nigeria ilifanya mazungumzo na kundi la waasi wa Niger Delta la kusini mashariki mwa nchi hiyo kwa upatanishi wa mashirika ya kigeni na jeshi la polisi kwa lengo la kulitafutia ufumbuzi tatizo la ukosefu wa amani ambalo limeathibiri vibaya eneo hilo kwa muda mrefu sasa.

Uharibifu wa mabomba ya mafuta mara nyingi hufanyika kwa lengo la kuiba mafuta hayo, na jambo hilo limekuwa la kawaida sana nchini Nigeria, ambayo ni mzalishaji mkuu wa mafuta ghafi barani Afrika.

Waziri wa Mafuta wa Nigeria amesema, mazungumzo baina ya serikali na waasi yamekuwa na mafanikio makubwa. Amesema, malengo ya mwaka 2017 ya nchi yake ni kumaliza kabisa vitendo vya uharibifu vinavyofanywa na makundi mbalimbali ya nchi hiyo.
Sehemu kubwa ya mafuta ghafi ya Nigeria yanazalishwa katika eneo la Niger Delta la kusini mashariki mwa nchi hiyo. 

Asilimia 80 ya bajeti ya Nigeria inategemea uuzaji nje mafuta ghafi ya nchi hiyo.